Taarifa ya Habari 26 Septemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Waziri Mkuu Scott Morrison anasisitiza kuwa viongozi wamjimbo, wana wajibu wakufungua mipaka yao, wakati 80% ya umma itakapokuwa ime pata chanjo kamili.


Maeneo ya kanda ya Victoria yatashiriki katika majaribio 20 yakuruhusu kumbi, kuwahudumia idadi kubwa ya wateja ambao wame pata chanjo kamili. Majibio ya kanda yatafunika sehemu kama mahoteli, vinyozi, utalii, mashindano ya farasi pamoja na matamasha.

Wajerumani milioni 60.4 wanapiga kura kuchagua wabunge na chama kitakachokuwa na ridhaa yao kumuweka Kansela mpya. Wajerumani leo 26.09.2021 wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wenye ushindani mkali kati ya vyama vikuu viwili,Social Democratic kinachoongozwa na Olaf Scholz na kile cha muungano wa kihafidhina cha Christian Democratic Union/Christian Social Union-CDU/CSU kikiongozwa na Armin Laschet.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema vikosi vya serikali yake vitasaidia kuhakikisha hali ya usalama na kujenga tena maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji, yaliyoharibiwa na waasi wa Kiislamu. Kagame alisema hayo Ijumaa wakati maafisa wa serikali ya Msumbiji wakianza kuhamasisha raia wa nchi hiyo kurudi makwao katika eneo hilo lenye utajiri wa gesi. Umoja wa Mataifa umeonya juu ya tishio linaloendelea la wanamgambo huko Cabo Delgado, ambako vikosi vya Rwanda vinashika doria katika barabara zilizotelekezwa na waasi ambao kwa wakati mmoja walikuwa wanazingira.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service