Taarifa ya Habari 26 Septemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Daniel Andrews ametangaza uamuzi wake wakujiuzulu kama kiongozi wa Victoria.


Bw Andrews alitoa tangazo hilo katika hotuba ya ghafla kwa vyombo vya habari mapema hii leo nje ya bunge, ambako mkewe Cath alisimama kando yake. Baada ya takriban muongo katika kazi hiyo, Bw Andrews amesema huu ndiwo wakati waku jiuzulu.

Mmoja wa viongozi wa kampeni ya La, Nyunggai Warren Mundine ame ishtumu serikali ya Albanese kwa kutaka kurejesha ubaguzi wa rangi ndani ya katiba. Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari mjini Canberra mapema hii leo, Bw Mundine aliwahamasisha wa Australia wapige kura ya la katika kura ya maoni ijayo kwa sauti yawa Australia wa asili bungeni, akisema Kauli ya Uluru kutoka moyoni ni ishara ya tangazo la vita. Ameongezea kuwa wa Australia watakuwa na chaguzi watakapo ingia debeni 14 Oktoba 2023.

Somaliland imesema haina mpango wa kufanya mazungumzo ya kujadili umoja, baada ya rais Yoweri Museveni kutoa pendekezo la kuwa mpatanishi kati ya nchi hiyo inayojitangazia jamhuri na serikali ya shirikisho ya Somalia. Rais Museveni jumamosi alisema kwamba amekubali kuchukua jukumu la mpatanishi wa amani baina ya makundi mawili baada ya Mkutano na mjumbe wa serikali ya Somaliland mjini Entebe nchini Uganda.

Marekani na Kenya wamesaini makubaliano ya ulinzi yatakalisaidia taifa hilo la Afrika Mashariki kupata vifaa na msaada kwa wanajeshi wakati taifa hilo likijiandaa kuongoza ujumbe wa kimataifa wa amani nchini Haiti. Haiti inapambana na machafuko yanaoyasababishwa na makundi ya uhalifu na hasa katika mji mkuu Port-au-Prince. Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesaini makubaliano hayo na mwenzake wa Kenya Aden Duale katika mkutano uliofanyika Nairobi.

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, amekashifu kile ambacho amesema ni habari za kupotosha kuhusu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye taifa lake wakati akiwa nje ya nchi kwa kipindi cha wiki mbili. Rais Ndayishimiye amekuwa nchini Cuba kwa ziara na kuzuru pia kule nchini Marekani ambako alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Siku moja baada ya kiongozi huyo wa nchi kuondoka nchini mwake tarehe 10 ya mwezi Septemba, taarifa ziliaanza kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwepo kwa njama ya kutekelezwa kwa mapinduzi dhidi yake. Hadi sasa chanzo cha taarifa hizo za kupotosha bado hakijatambuliwa.




Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service