Serikali ya Magharibi Australia, yatoa vipimo vya RAT kwa familia za Magharibi Australia, katika juhudi yaku kabiliana na wimbi la maambukizi ya virusi vya Omicron. Viongozi wa majimbo ya New South Wales na Queensland, waomba watu watii onyo za mafuriko na waache kuhatarisha maisha yao kwa kuendesha magari katika maji ya mafuriko.
Marais saba wa nchi za Afrika walikusanyika mjini Kinshasa siku ya Alhamis kutathmini makubaliano ya mwaka 2013 yaliyolenga kuimarisha amani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika eneo la mashariki lililokumbwa na ghasia na eneo la maziwa makuu. Muundo wa amani, usalama, na ushirikiano unalenga kukuza juhudi za kuleta utulivu katika kanda. Mamilioni ya watu walikufa kutokana na ghasia, magonjwa, au njaa katika vita vya Congo vya mwaka 1996 hadi 1997 na mwaka 1998 hadi 2003 katika vita vya Congo mzozo ambao ulikumba mataifa katika eneo la Afrika mashariki na kati.
Chama tawala cha Kenya, Jubilee kimetangaza kumunga mkono Raila Odinga, kiongozi mkongo wa upinzani katika juhudi zake za kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi mkuu wa Ogusti mwaka huu. Uamuzi huo unamuondoa Naibu Rais William Ruto kuwa mgombea wa chama hicho.