Bw Frydenberg ana ahidi mfuko wa msaada wa fedha kuwasaidia wa Australia, kukabiliana na ongezeko ya gharama ya maisha. Mweka hazina ameongezea pia kuwa hatua hizo zime undwa ili zisi ongeze shinikizo zaidi kwa mfumuko pamoja nakusababisha ongezeko la mapema la kiwango cha riba kutoka kwa benki kuu.
Wakaaji wa Queensland wana onywa wajiandae kwa hali mbaya ya hewa, wakati hali ya hewa hatari ina pita katika eneo la kusini mashariki ya jimbo hilo. Ofisi ya utabiri wa hewa imesema, mvua nyingi nzito pamoja na mafuriko yakutishia maisha yako njiani. Wakati huo huo, mvua nyingi inatarajiwa kuathiri maeneo ya kaskazini New South Wales. Huduma ya dharura ya jimbo hilo ime sema, watu wanastahili kuwa tayari kufuata ushauri na kuhama maeneo husika iki hitajika.
Kaya mbalimbali nchini Kenya zinakabiliwa na ukata wa kifedha baada ya bei za bidhaa muhimu kupanda kutokana na ongezeko la mfumuko wa bei, na kudhoofisha shilingi na kupandisha joto la Uchaguzi Mkuu Agosti 9. Wachambuzi wa taasisi ya kifedha AZA Finance, wamesema ongezeko la mfumuko wa bei kutokana kupanda kwa bei za bidhaa katika soko la kimataifa limechangia sana katika sarafu ya eneo iliyodondoka kufikia kiwango kipya cha chini cha Ksh 114.55($1) dhidi ya dola wiki iliyopita kutoka Ksh114.33 wiki iliyopita. Hali hiyo imechangiwa nahatua ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta kuongeza bei ya mafuta (petroli na diseli) kwa Ksh5 ($0.04) kwa lita.