Hatimae muswada wa mawasiliano ya viwanda wa serikali ya shirikisho kupitishwa bungeni, baada yakuungwa mkono na mmoja wama seneta huru.
Kundi la waasi wa M23 Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Ijumaa limesema linataka kufanya mazungumzo na Serikali baada ya rais wa Congo na viongozi wengine wa Afrika kutia saini makubaliano ya kusitisha mapino na kuweka silaha chini yenye lengo ya kusitisha mashambulizi ya wanamgambo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amerefusha muda wa karantini kwa siku 21 zaidi katika wilaya mbili ambazo ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Rais Museveni amesema hatua za serikali ya Uganda za kupambana na ugonjwa huo zimepata mafanikio. Vikwazo vya kuingia na kutoka katika wilaya za Mubende na Kassanda zilizoko katikati mwa Uganda vitawekwa hadi kufikia Desemba 17.