Wapatanishi wanao ongozwa na Qatar, wana ongeza juhudi zaku ongeza muda wakusitisha mapigano. Binti wa miaka minne ambaye ni raia wa Marekani na Israel kwa jina la Abigail Edan, ni miongoni mwa mateka wa Israel na aliachwa yatima baada ya wazazi wake kuuawa na Hamas katika shambulizi la Oktoba 7.
Mike Pezzullo amefutwa kazi kama katibu wa wizara wa maswala ya nyumbani, baada ya uchunguzi kukamilika kwa kukiuka kanuni za maadili. Alisimamishwa kazi baada ya kashfa ya ujumbe mfupi wa simu, pamoja na kuvuja kwa ujumbe ulionesha kuwa katibu huyo, alifanya ushawishi kwa niaba ya idara yake mara kadhaa, na alipendekeza maoni yake binafsi katika ukiukwaji wa vigezi vya huduma, kwa muda wa miaka mitano. Taarifa iliyo tolewa na ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Albanese ilisema kuwa hatua hiyo ilifanywa kufuatia mapendekezo yaliyo fanywa na uchunguzi huru.
Serikali ya shirikisho inawekeza $225 milioni za ziada kwa mashirika ya ulinzi, ambayo ni Australian Federal Police na Australian Border Force, ambayo yata wafuatilia wafungwa wa uhamiaji ambao walikuwa ndani ya vizuizi vya uhamiaji. Watu wengine 45 wame achiwa huru pia kutoka vizuizi hivyo baada ya uamuzi wa mahakama ya upeo, kutoa hukumu kuwa kufungwa bila tarehe yakuachiwa huru ni kinyume cha sheria, hali ambayo ina leta idadi kamili ya watu walio achiwa huru kufikia 138. Uamuzi wa Mahakama kuu wa Novemba, unahitaji walio achiwa huru, kuwa chini ya masharti ya vizuizi pamoja na kuvaa vifaa vyaki elektroniki vyaku fuatiliwa milele.
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amesema hali ya utulivu imerejea nchini humo baada ya kutokea shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi kwenye mji mkuu wa taifa hilo mapema jana Jumapili. Akilihutubia taifa kupitia televisheni usiku wa kuamkia leo, rais Bio amesema wote waliopanga na kuongoza shambulizi hilo wamekamatwa na kwamba operesheni za usalama na uchunguzi wa suala hilo vinaendelea.
HUENDA ukuruba wa kisiasa uliokuwepo baina ya Gavana wa Kisii, Simba Arati na naibu wake, Dkt Robert Monda umeingia dosari kufuatia matukio ya hivi punde ambapo naibu huyo alikutana na wakosoaji wakubwa wa kisiasa wa bosi wake. Wakosoaji hao ambao ni wabunge Silvanus Osoro (Mugirango Kusini), Japheth Nyakundi (Kitutu Chache Kaskazini), Daniel Manduku (Nyaribari Masaba), Mwakilishi wa kina Mama Dorice Aburi na baadhi ya madiwani (MCAs) mnamo Novemba 25, 2023 walikutana na Dkt Monda katika boma lake lililoko kijijini Rigena, eneobunge la Nyaribari Chache nyakati za usiku. Japo viongozi hao waliwaambia wanahabari kuwa mkutano wao ulikuwa wa kutathmini jinsi ya kufanikisha maendeleo katika kaunti hiyo, ilionekana wazi kwamba viongozi hao walikuwa wakipanga njama kuhusu namna ya kumtenga Gavana Arati dhidi ya viongozi wengine wa gatuzi hilo.