China imetangaza leo kuziwekea vikwazo kampuni za silaha za Marekani baada ya Washington kuidhinisha mauzo ya silaha yenye thamani ya dola bilioni 1 kwa Taiwan.
Rasimu ya kurekebisha katiba ya Kenya yazinduliwa, rasimu hiyo inapendekeza kubuniwa nafasi ya rais, makam wa rais, waziri mkuu na manaibu wake wawili watakaoteuliwa na rais, pamoja na kiongozi wa upinzani.
Zoezi la upigaji kura ya mapema huko Zanzibar limeanza saa moja asubuhi. Kwa hii leo wanaopiga kura ni wa chache kwa sababu ya utaratibu uliopangwa. Kura hii ya mapema ni ya kwanza kabisa kufanyika huko visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.