Taarifa ya Habari 27 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Vita vya Israel na Hamas vimezua vita vya maneno kati ya chama cha Greens na serikali ya Labor pamoja na chama cha upinzani.


Watanzania wawili na raia mmoja wa Kusini ni miongoni mwa mateka 224 wanaoshikiliwa na Hamas baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 nchini Israel, serikali ya Israel inasema. Hakuna hata mmoja kati ya hao watatu aliyetajwa.

Onyo la dharura limetolewa kwa moto mkubwa unao sambaa kwa kasi karibu ya Mt Isa Kaskazini Queensland, wakaazi wa eneo hilo wame hamasishwa waondoke mara moja kwa sababu maisha yao yako hatarini. Shirika la dharura la Queensland Fire and Emergency Services, lime sema mali ime athiriwa na wazima moto huenda wasiweze zuia moto huo kuendelea kukaribia, wakionya kuwa hivi karibuni itakuwa hatari sana kuendesha magari katika eneo hilo. Onyo hilo nikwa Lake Moondarra Road, Barramundi Way, The Junction, na mbuga za karibu ya Lake Moondarra, shirika la Queensland Fire and Emergency Services lili sema mapema hii leo Ijumaa.

Waziri wa maswala yawa Aboriginal wa jimbo la New South Wales, amesema anatumai kupitisha sheria zakuweka mchakato wa mashauriano ya mkataba kabla ya uchaguzi ujao. Jimbo hilo ni miongoni mwa mamlaka ya mwisho nchini Australia, kuanza mchakato wakuwa na mkataba licha yakuwa na idadi kubwa yawa Australia wa kwanza kuliko jimbo lingine nchini Australia. New South Wales ni nyumbani kwa idadi 278,000 yawa Aboriginal na wanavisa wa Torres Strait Islander pamoja na lugha 35 zaki Aboriginal.

Uchunguzi ulifunguliwa siku ya Alhamisi uliopewa mamlaka ya kubaini jukumu kwenye moto huko Johannesburg ambao ulisababisha vifo vya watu 77, na kuangazia magenge ambayo yanateka majengo yaliyotelekezwa katikati ya jiji na kuyakodisha kinyume cha sheria.

Taifa la Sudan barani Afrika limegubikwa na mzozo mkubwa sana wa wakimbizi wa ndani duniani. Takriban watu milioni 5.6 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan baada ya mapigano ya zaidi ya miezi sita, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu. Watalam wa masuala ya kutetea haki za binadamu wanahofia kuwa nchi hiyo huenda ikatumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service