Serikali ya Marekani ina mipango ya kuwadhibiti wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na kwingineko duniani, kwendelea na masomo kwenye vyuo vikuu nchini humo, kwa kuweka masharti mapya ya viza, ambayo yatadhibiti ukazi wao.
Mgombea urais nchini Tanzania Tundu Lissu wa chama cha Chadema, amesema endapo atachaguliwa kuwa rais kutakuwa na "uhuru kamili" wa vyombo vya habari bila kusimamiwa au kuingiliwa na serikali.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa onyo kali kwa waziri wake wa ulinzi Nosiviwe Mapisa - Nqakula na kusimamisha mshahara wake kwa miezi mitatu kwa kupeleka ujumbe nchini Zimbabwe kwa ndege ya jeshi la anga. Haya ni kwa mujibu wa ofisi ya rais.