Serikali ya Labor imezindua kampeni yake yakuanzisha tume ya shirikisho yakukabiliana na ufisadi. Serikali imesema ita ahidi uwekezaji wa dola milioni $262 kwa muda wa miaka minne, kuhakikisha tume hiyo inarasilimali yakutosha kudumisha uadilifu katika maisha ya umma.
Akaunti inayo dai kuhusika na udukuzi wa data za Optus, imeomba radhi nakusema imeondoa tisho lake lakuteka nyara data zawatumiaji. Akaunti hiyo ya mtandaoni iliyo toa tisho hizo, inaaminika kuwa ni halali na wataalam wa usalama wa mtandaoni ila, bado haija thibitishwa na Optus pamoja na Jeshi la polisi la shirikisho. Akaunti hiyo mwanzoni ilitishia kuchapisha data zaidi za wateja, kama Optus haita ilipa $1.5 milioni ((AUD)).
Idadi ya watu waloambukizwa na ugonjwa wa Ebola inazidi kuongezeka nchini Uganda. Wizara ya afya inasema kumekuwa na watu 34 wanaodhaniwa wameambukizwa na virusi hivyo vya hatari. Inaamini kwamba watu 21 wamefariki kutokana na Ebola. Nchi jirani zimesema ziko katika hali ya tahadhari kubwa.