Muswada huo wenye thamani ya dola bilioni 10 kwa jina la Housing Australia Future Fund, imekwama ndani ya seneti tangu machi chama cha Greens and chama cha mseto viki kata kuunga mkono.
Alipo zungumzia muswada huo Waziri Mkuu Anthony Albanese, alisema madai ya chama cha Greens kwa kusitisha kwa ongezeko ya kodi ya nyumba haiwezekani kwa sababu hiyo ni jukumu ya serikali ya jimbo. Naibu kiongozi wa chama cha Liberals, Sussan Ley amesema muswada huo wa nyumba hauja pitishwa ndani ya seneti kwa sababu ni muswada mubaya.
Waziri wamaswala yakigeni wa Australia Penny Wong, amesema usalama na ushirikiano katika kanda ya pasifiki, itakuwa juu katika ajenda, pamoja na mazingira katika mazungumzo ya AUSMIN. Waziri wa maswala yakigeni wa Marekani pamoja na Waziri wa Ulinzi walikutana na washiriki wao wa Australia, kabla ya kufanya mkutano na Waziri Mkuu Ijumaa. Seneta Wong ame eleza shirika la habari la A-B-C kuwa Marekani, ina mahusiano ya kina katika kanda hili.
Wanasayansi wamesema julai ina elekea kuwa mwezi wenye joto zaidi katika rekodi za dunia. Shirika la utabiri wa hali ya hewa la umoja wa mataifa na huduma ya mabadiliko ya hewa ya muungano wa ulaya ya Copernicus, yamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa, mwezi huu utavunja rekodi za joto. Alipo zungumzia hoja hiyo, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, alisema data iliyo tolewa na mashirika yako sambamba na utabiri wa mabadiliko ya hali ya hewa na, madhara kwa watu yatakuwa mabaya.
Mahakama ya Rufaa ya Kenya imebatilisha amri iliyotolewa mwezi uliopita ya kusimamisha kwa muda utekelezwaji wa sheria mpya ya fedha ya 2023, baada ya waziri wa Fedha Prof Njuguna Ndung’u kusema kwamba serikali inapoteza nusu bilioni kila siku kutokana na hatua hiyo. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Ijumaa, jopo la majaji watatu wa Rufaa limeondoa amri hiyo iliyowekwa Juni 30, wakati rufaa iliyowasilishwa na waziri Ndung’u ikisubiriwa. Awali Ndung’u kupitia kwa mwanasheria mkuu wa Kenya, Justin Muturi aliwasilisha rufaa mahakamani akisema kwamba serikali huenda ikapoteza takriban shilingi bilioni 211, ndani ya mwaka huu wa kifedha iwapo sheria hiyo itasitishwa.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Ijumaa amewasili kwenye mji mkuu wa jimbo la Sichuan, wa Chengdu, kusini-magharibi mwa China, ili kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa michezo ya 31, ya shirikisho la michezo ya vyuo vikuu vya kimataifa, FISU, pamoja na kutembelea China. Hiyo ni ziara ya kwanza ya Ndayishimiye nchini China baada tangu aliposhika madaraka Juni 2020. Msafara wake unashirikisha waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa maendeleo, waziri wa mazingira, kilimo na mifugo, pamoja na maafisa wengine wa serikali. Mara kwa mara, rais huyo amekuwa akisema kuwa Burundi inaichukulia China kama rafiki, na mfano mzuri, akielezea kuwa nchi yake ingependa kuendelea kuimarisha urafiki na ushirikiano na taifa hilo, ili kupata maendeleo ya pamoja.
Na katika michezo, sherehe zaendelea katika jamii yawa Naijeria wanao ishi Australia baada ya timu yao ya kina dada Super Falcons kuicharaza Matildas ya Australia, katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la FIFA.