Shirika la tamaduni nyingi nchini Australia, limesema sensa ya 2021 imeonesha kuwa utofauti ume chipuka na umekuwa sehemu pana ya jamii nchini Australia. Ofisi ya takwimu ya Australia almaarufu (A-B-S) imetoa data kutoka sensa mpya inayo onesha kuwa takriban nusu ya umma ya Australia 48.2%, ni wahamiaji wa vizazi wa kwanza au wapili na wana mzazi angalau mmoja aliye zaliwa nga'mbo. Pia dini laki hindu naki Islamu ni dini zinazo kuwa kwa kasi nchini Australia dini laki hindu likikuwa kwa 2.7% na dini laki Islamu liki kuwa kwa 3.2%.
Ripoti mpya imesema kuna uhaba wa takriban elfu 35 yawafanyakazi wa huduma ya wazee mwaka huu. Takwimu hiyo imeongezeka mara mbili tangu uhaba wa mwaka jana, ambapo idadi hiyo ilikuwa uhaba wa wafanyakazi takriban elfu 17. Kamati ya uchumi na maendeleo almaarufu (CEDA), iliyo toa matokeo ya utafiti huo mapema hii leo jumanne 28 Juni, imesema hakuna wafanyakazi wakutosha waku kidhi mahitaji ya msingi ya huduma iliyopendekezwa na tume yakifalme kwa huduma ya wazee.
Msemaji wa jeshi la Sudan Nabil Abdullah amesema Jumatatu kupitia ujumbe wa video kwamba jeshi la Ethiopia limeua wanajeshi 7 wa Sudan pamoja na raia mmoja waliokuwa wameshikiliwa mjini Addis Ababa. Taarifa hiyo ndiyo ya karibuni zaidi inayoashiria kudorora kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Abdullah ametaja mauaji hayo kutekelezwa na waoga, akiongeza kwamba Khartoum itajibu vilivyo.