Jimbo la Queensland limerekodi kesi ya tatu ya COVID-19 ndani ya jamii, wakati jeshi la polisi lina sahihisha maelezo kuhusu mkusanyiko ulio fanywa na kesi iliyo thibitishwa. Uchunguzi wa ziada wa polisi wa Qld umesema kuwa, mhusika alikuwa nawageni watano katika sherehe ndani ya nyumba, nasi watu 25 kama ilivyo ripotiwa kabla.
Kiongozi wa chama cha Labor kitaifa Anthony Albanese amesema mbunge wa jimbo la Qld Andrew Laming, lazima ajiuzulu kutoka bungeni maramoja. Mbunge huyo Bowman wa chama cha LNP amesema hatawania uchaguzi mkuu ujao, baada ya tabia isiyo faa kwa wanawake katika mitandao yakijamii.
Rais Uhuru Kenyatta, katika hotuba yake Ijumaa mchana, ameeleza Kenya imeripoti ongezeko la maambukizi ya Covid-19. Kiwango hiki ni cha juu zaidi kuliko wakati janga hilo lilipoanza. Ameamuru kusitishwa vikao vya kawaida vya bunge la Agosti, na mabunge ya kwenye kaunti za Nairobi, Machakos, Kajiado, Kiambu na Nakuru na kamati zake zote.