Chama cha Labor kimetoa rasimu ya mkakati wakitaifa kwa sekta za huduma ya Australia, kikiapa kukarabati sekta ya huduma yawazee, walemavu, maveterani na mfumo elimu yamapema ya watoto. Mkakati wa rasimu hiyo unasema kuona viwango vya juu vya wato wanao ondoka katika sekta hizo kwa sababu, ya malipo duni na kuto tambuliwa kwa kazi hizo, mwendelezo mdogo wa taaluma, viwango vya juu vya majukumu na wakati mwingine mazingira yasiyo salama ya kazi.
Marekani na Saudi Arabia zimetoa mwito kwa pande hasimu nchini Sudan kuongeza muda wa kusimamisha mapigano utakaofika kikomo kesho Jumatatu. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mapema leo, Washington na Riyadh zimesema kurefushwa kwa muda wa kuweka chini silaha kutawezesha utoaji wa misaada ya kiutu ya haraka inayohitajika kwa watu wa Sudan.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna wanajeshi waliopoteza maisha katika shambulio lililofanywa na kundi la Al Shabaab, dhidi ya kambi ya jeshi la walinda amani wa Umoja wa Afrika kutoka Uganda nchini Somalia. Kwenye taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la Reuters, Museveni hakutaja idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa au kuuwawa.