Taarifa ya Habari 29 Agosti 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese, ajiaandaa kutangaza tarehe ya kura ya moani kwa Sauti yawa Australia wa Kwanza bungeni.


Madaktari jimboni Victoria wanaiomba serikali izingatie tena mageuzi kwa sheria ya kodi mpya inayowalenga ma GP. Mapema mwezi huu, ofisi za ushuru zamajimbo ya New South Wales na Victoria, waliamua kuwa mapato yama GP ya kiwango fulani kwa sasa yatakabiliwa kwa kodi ya 5.45% na 4.85% pia. Madaktari wamekadiria kuwa nyongeza hiyo ya ushuru inaweza wagharimu wagonjwa $20 za ziada kwa miadi, nama GP wanahofu watalazimishwa kufunga milango yao watakapo kabiliwa kwa kodi zitakazo daiwa miaka tano ya nyuma.

Zaidi ya wataalam 1,000 wa afya wakiwemo mawaziri kutoka mataifa ya Afrika wanakutana Botswana kwa mkutano wa kikanda wa Shirika la kimataifa la Afya, WHO.
Wanaohudhuria wanalenga kuhakikisha kwamba Afrika imejiandaa vilivyo kutokana na majanga katika siku za nyuma, kinyume na ilivyokuwa wakati wa janga la corona.

Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi yuko mjini Kinshasa kujadili masuala ya maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili wiki chache baada ya mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioafanyika Bujumbura. Miongoni mwa masuali ambayo Felix Tshisekedi na Evariste Ndayishimiye waliyagusia ni pamoja na amani, uhusiano na biashara.

Afrika Kusini na Marekani zimetilia maanani ripoti za waangalizi wa uchaguzi nchini Zimbabwe na kutoa wito wa amani baada ya upinzani nchini humo kudai uwepo wa udanganyifu katika kura. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake imezingatia ripoti ya waangalizi wa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC juu ya uchaguzi uliokamilika wa Zimbabwe, na kuzitaka pande zote nchini humo kushirikiana.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service