Shirika hilo la kimataifa linalo wahudumiwa wakimbizi waki Palestina, UNWRA, limefuta kazi wafanyakazi kadhaa kutoka nguvu kazi yake yenye wafanyakazi elfu 13 mjini Gaza, na uchunguzi kwa madai hayo una endelea. Shutma hizo zime fanya Australia, Canada, Britain, Italy, Germany, France na Japan kusitisha au kuzuia misaada yao, kwa shirika hilo la UNWRA na Marekani nayo pia imesitisha msaada wayo.
New South Wales itapiga marufuku saluti zaki Nazi, baada ya wazungu wabaguzi wa rangi kufanya maandamano kadhaa mjini Sydney kwa siku tatu mfululizo. Kiongozi wa jimbo hilo Chris Minns, amepongeza jeshi la polisi kwa kuvunja mikutano hiyo pamoja nakutoa amri ya usalama wa umma ila, ame ongezea kuwa sheria za sasa lazima zi imarishwe. Wakati ishara zaki Nazi zimepigwa marufuku jimboni New South Wales, tofauti na jimboni Victoria hakuna sheria inayo piga marufuku saluti zaki Nazi.
Mataifa ya Afrika Magharibi ya Mali, Burkina Faso na Niger yamejiondoa kwenye shirika la kiuchumi la kieneo la ECOWAS, viongozi wao wa kijeshi wamesema Jumapili.
Wote wamelaumu ECOWAS kwa hatua kandamizi za kuwawekea vikwazo, kama njia ya kuwalazimisha kuachana na mapinduzi yaliofanyika kwenye mataifa yao. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ECOWAS kupitia taarifa imesema kwamba haijafahamishwa rasmi kuhusu uamuzi wa mataifa hayo. Viongozi wa kijeshi wa mataifa hayo kupitia taarifa ya pamoja iliyosomwa kupitia televisheni zao zote za kitaifa, wamesema kwamba,” wamemua kupitia utaifa wao kamilili kujiondoa mara moja kwa Burkina Faso, Mali na Niger kuondoka ECOWAS, “ wakidai kuwa shirika hilo limeondoka kwenye malengo ya waanzilishi wake pamoja na wanaharakati wa Umoja wa Afrika, baada ya kuwepo kwa karibu miaka 50 tangu kubuniwa.
Uganda imejitenga na maoni yaliyoandikwa na jaji wa nchini humo Julia Sebutinde ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ katika dhidi ya Israel.
Serikali ya Uganda kupitia taarifa yake imesema kwamba msimamo uliochukuliwa na Jaji Sebutinde ni wake binafsi, na hauakisi kwa njia yoyote nafasi ya serikali ya Jamhuri ya Uganda. Aidha iliongeza kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki inaunga mkono msimamo wa vuguvugu la mataifa yasiyofungamana na upande wowote kwenye mzozo huo, uliopitishwa katika mkutano mkuu uliofanyika katika mji mkuu Kampala mwezi huu.