Ndege hiyo ilikuwa ikishiriki katika mazoezi yakijeshi yaliyo fanywa usiku katika mazoezi ya Talisman Sabre iliyo husu helikopta mbili, ilipo fanya ajali karibu ya pwani ya Queensland mida ya saa tanu usiku wa Ijumaa. [[JULY 29]]
Talisman Sabre ni mazoezi yakijeshi ya wiki mbili yanayo jumuisha vikosi elfu 30 kutoka nchi 13. Waziri wa Ulinzi Richard Marles amesema familia za wanahewa wanne walio husika katika ajali hiyo, wame arifiwa na fikra na mawazo yake yako kwa timu zinazo husika katika juhudi hizo zakutafuta na uokozi.
Chama cha Greens kina simama wima kwa madai yacho, kikiwa kime kata kuunga mkono mfuko wa serikali ya shirikisho wenye thamani yamabilioni ya dola kwa ujenzi wa nyumba kama matakwa yao hayata tekelezwa. Waziri Mkuu Anthony Albanese ame hamasisha chama cha Greens kiunge mkono mradi huo wa ujenzi wa nyumba, au kitakuwa katika hatari yaku warejesha wapiga kura debeni mapema. Hata hivyo chama cha Greens, kime andika barua ya wazi kwa Bw Albanese, aliyosema wata unga mkono muswada huo tu kama serikali inakubali masharti kadhaa yanayo jumuisha kusitisha kuongeza kodi pamoja na ahadi yakuwekeza bilioni $2.5 kwa nyumba za umma naza bei nafuu. Serikali ya shirikisho inatarajiwa kuwasilisha tena muswada huo bunge litakapo anza vikao tena wiki ijayo ila, ukikatiliwa tena Bw Albanese amesema tisho lakufunga bunge na kuitisha uchaguzi mkuu bado lipo.
Viunganisho vya gesi vinatarajiwa kupigwa marufuku, katika nyumba zote zinazo jenga jimboni Victoria kuanzia mwezi ujao. Kuanzia januari mosi 2024, nyumba zote mpya zamakaazi pamoja na zinazo jengwa kando ya nyumba hizo zita hitaji kibali cha upangaji na zita tumia umeme pekee.
Lily D’Ambrosio ni Waziri wa Nishati wa jimbo hilo, amesema mageuzi hayo yatasaidia Victoria kufikia lengo lake la uzalishaji sufuri wa kaboni kufikia mwaka wa 2045.
Jenerali Abdourahmane Tchiani amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa taifa la Nijer, baada ya mapinduzi yakijeshi. Kiongozi hiyo wa kundi la wanajeshi lililo pindua serikali, nakumfunga rais aliye chaguliwa kidemokrasia, ali hotubia taifa hilo Julai 28 siku mbili baada ya jeshi kuchukua mamlaka. Jenerali Tchiani, ambaye hutumia jina la Omar pia amesema nchi hiyo inahitaji kubadilisha mwelekeo wayo, ili kupata uhifadhi wayo na kuwa yeye pamoja na wengine wali amua kuingilia kati kukabiliana na changamoto zakiuchumi, usalama na kijamii. Jenerali Omar ameongezea kuwa alizungumza kwa niaba ya baraza lataifa, kwa ulinzi wa nchi hiyo [[CNSP]], kundi la wanajeshi linalo dai uwajibikaji kwa kufanya mageuzi hayo. Aliongezea pia kuwa C-N-S-P ina nia yaku Heshimu makubaliano yote yakimataifa, ambayo jamuhuri ya Nijer imetia saini, pamoja na haki za binadam.
Umoja wa Ulaya hatimaye umeanzisha mfumo maalum wa vikwazo vinavyowalenga wahusika wakuu katika vita vya Sudan vinavyoendelea, kwa kuwawekea vizuizi vya kusafiri na mali zao ikiwemo kuwafungia akaunti za benki, vyanzo vya kidiplomasia vinavyofahamu suala hilo vimesema. Hati ya pendekezo iliyotumwa kwa nchi wanachama mwishoni mwa wiki iliyopita, na maelezo zaidi kuhusu suala hilo yatajadiliwa wiki zijazo, vyanzo vya kidiplomasia vilisema. Lengo ni kumaliza muundo wa kazi ifikapo Septemba, baada ya hapo unaweza kutumika kutengeneza orodha ya watu binafsi na makampuni yaliyopigwa marufuku, vyanzo vilisema. EU tayari imeyawekea vikwazo mashirika na watu binafsi wanaohusishwa na kundi la mamluki la Wagner la Russia, linaloongozwa na Yevgeny Prigozhin, zikiwemo shughuli zake nchini Sudan pamoja na makampuni mawili ya dhahabu.
Katika michezo:
Ulinganisho kati ya Erling Haaland na Rasmus Hojlund uko wazi. Wote wana urefu wa futi 6 na rangi ya nywele zao inafanana. Wote wawili hawana huruma wakati wa kushambulia. Mwanzoni mwa msimu mpya wa Ligi Kuu, wote wanaweza kuwa wanacheza vilabu vya Manchester. Akizungumza siku ya Jumatatu, meneja wa United, Erik ten Hag alisema klabu hiyo imepiga hatua kutafuta mshambuliaji mpya. Hojlund, 20, anasalia kuwa shabaha ya wazi zaidi ya United, ingawa Mashetani Wekundu wanasita kufikia dau la Atalanta la pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark.