Vikundi vya watetezi wa walemavu vimewasili mjini Canberra kabla ya kutangazwa kwa bajeti, kukabidhi barua ya wazi kwa bunge inayo omba mageuzi yafanywe kwa mfumo wa NDIS. Kundi hilo liliwasilisha barua hiyo kwa kiongozi wa chama cha Labor Anthony Albanese pamoja na msemaji wa NDIS katika upinzani Bill Shorten mapema leo jumanne. Barua hiyo iliwaomba viongozi hao wa ahidi kurejesha mfumo huo katika hali yake ya zamani.
amri saba zaku hama zimetolewa katika eneo la kaskazini za jimboni la New South Wales, hali baada ya hali mbaya ya hewa kurejea katika kanda hiyo. Huduma ya dharura ya jimbo hilo imesema inatarajia mafuriko wastan katika mji wa Lismore, haswa katika maeneo ambayo yalikabiliwa kwa mafuriko mwezi ulio pita. Ofisi ya utabiri wa hewa nayo imetabiri kuwa maeneo ya Coffs Harbour, Hawkesbury na Greater Sydney yata athiriwa sana.
Mahakama nchini Kenya Jumatatu imewaachilia huru waendesha boda boda 16 waliokamatwa kutokana na shambulio baya dhidi ya mwanadiplomasia wa kike, baada ya serikali kushindwa kutoa ushahidi wowote dhidi yao. Mwanaume wa 17, anayedaiwa kuwa kiongozi wa shambulizi hilo, ataendelea kukabiliwa na kesi na anakabiliwa na kifungo cha maisha jela ikiwa atakutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono. Alikamatwa wiki mbili zilizopita karibu na mpaka wa Tanzania, kwenye umbali wa kilomita 430 kaskazini magharibi mwa Nairobi baada ya kukwepa kukamatwa kupitia mrefeji wa maji taka, polisi walisema.