Taarifa ya Habari 29 Mei 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese asalia na masaa 24 kujua kama ataongoza serikali ya wengi, tume ya uchaguzi ya Australia ikiwa inaelekea kukamilisha hesabu za kura za maeneo bunge tatu ya mwisho.


Mbunge wa chama cha Liberal Karen Andrews amesema, anawaunga mkono Peter Dutton na Sussan Ley [[Lee]] ambao wamependekezwa kama viongozi wapya wa chama cha Liberal, watakapo idhinishwa kwenye mkutano wa chama cha Liberal saa tatu asubuhi ya Jumatatu 30 Mei. Chama cha The Nationals nacho kitafanya mkutano kesho Jumatatu asubuhi, kumchagua kati ya David Littleproud na Darren Chester ambao wana wania uongozi wa chama hicho dhidi ya kiongozi wa chama hicho Barnaby Joyce.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imemuita balozi wa Rwanda and kusimamisha safari za Rwandair kwenda Congo ikiwa ni majibu kwa kile ambacho inasema uungaji mkono wa Kigali kwa waasi wa M23 wanaofanya mashambulizi ya kijeshi mashariki mwa Congo. Rwanda imekanusha kuwasaidia waasi, ambao wamekaribia kiasi cha kilometa 20 wiki hii huko mashariki mwa Congo kuelekea mji wa Goma, na kwa muda mfupi walikamata kambi kubwa ya kijeshi katika eneo hilo.

Kiongozi wa Chama cha Wiper nchini Kenya, Kalonzo Musyoka hatashiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Rais Agosti 9 baada ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kumzuia kugombea kutokana na utaratibu uliopo. Wakati huo huo, Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) imewapitisha wagombea 16 ambao hivi sasa watawasilisha nyaraka zao za uteuzi wao kuanzia Jumamosi. Orodha hiyo ina wagombea watarajiwa 9 wa vyama vya siasa au muungano wa vyama vya kisiasa na wagombea saba huru.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service