Kufikia Jumamosi Israel haikuwa imetoa tamko lolote kuhusiana na shutuma za kuhusika kwa kifo cha mwanasayansi wa masuala ya nyuklia wa Iran Mohsen Fakhrizade. Israeli iliwahi kumshtumu mwanasayansi huyo kwa kuhusika na mpango wa kisiri wa kuunda silaha za nyuklia.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema majeshi ya nchi hiyo yamechukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle. Abiy ametangaza kuwa serikali ya shirikisho sasa imechukua udhibiti kamili wa mji huo ikiwemo uwanja wa ndege, taasisi za umma, ofisi za utawala wa jimbo hilo na maeneo mengine muhimu.
Polisi nchini Uganda imeanza kufanya uchunguzi wa ghasia za ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wiki iliyopita zilizo sababisha vifo vya takriban watu 45, gazeti la Uganda la 'Daily Monitor' limeripoti. Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema uchunguzi huo unazingatia zaidi makosa yaliyo sababisha uharibifu.