Chama cha Greens kimeomba kusitishwa mara moja kwa kodi za nyumba pamoja namwisho wa kufukuzwa ndani ya nyumba bila sababu, kukabiliana na janga la uwezo wakumudu nyumba nchini Australia. Hali hiyo imejiri wakati ripoti mpya, iwezo wakukodi nyumba kila mwaka, imepata kuwa kodi zinaongezeka haraka kuliko mapato ya nyumba kote nchini, hali ambayo imewaacha watu wengi wakihangaika kupata sehemu yakuishi au, kuendelea kumudu wanako ishi.
Jamii katika jimbo la Kusini Australia zimeonywa zijiandae kwa dharura yamafuriko, wakati maji kutoka maeneo ya majimbo ya mashariki ya New South Wales na Victoria.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameelezea matumaini yake kuwa mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaweza kutatuliwa ikiwa michakato inayohusika itafikia sababu kuu ya mzozo huo. Hata hivyokundi la waasi la M23 siku ya Ijumaa lilikaidi wito wa kusitishwa kwa mapigano, likitaja mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa jeshi la Congo, FARDC, lakini wakaomba kukutana na mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Uhuru Kenyatta na Rais wa Angola Joao Lorenco, kutetea kesi yao.