Mweka hazina kivuli Jim Chalmers amesema hapatakuwa ongezeko ya kodi kama chama cha Labor kinashinda uchaguzi wa Mei, isipokuwa mpango wake ambao umewekwa wazi kufanya kazi na nchi zingine zinazo lenga mashirika yakimataifa.
Kundi la waasi la M23 linaloshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kusitisha mapigano, baada ya siku kadhaa za makabiliano makali na jeshi la kitaifa la DRC, msemaji wake amesema kupitia taarifa. Kundi hilo limesema linataka fanya mazungumzo na serikali na kwamba limewaondoa wapiganaji wake katika eneo la mapigano, ili kuepusha makabiliano mapya na jeshi la Kongo.
Shirikisho la kimataifa la Msalaba Mwekundu, limesema kwamba Juhudi za kufikisha misaada ya dawa katika eneo la Tigray, lililokumbwa na vita, zimeshindikana. Hii ni licha ya sitisho la mapigano kati ya serikali na majeshi ya Tigray, ya kuruhusu misaada kuingia sehemu hiyo.