Waziri wa elimu wa NSW amehamasisha chama cha walimu cha jimbo hilo, kifute mgomo wa kesho akiahidi kuwa bajeti ya mwezi ujao utashughulikia mishara ya sekta ya umma. Ila rais wa chama cha walimu cha NSW Angelo Gavrielatos, amesema mgomo utafanyika ulivyo ratibiwa walimu wanapo omba nyongeza kwa mshahara wao kutoka 5% hadi 7.5%.
Mamlaka ya magereza nchini Morocco imekuwa ikitoa mafunzo ya kutokomeza ugaidi tangu mwaka 2017 kwa wapiganaji wa zamani wa kundi la Islamic State (IS) na wengine waliopatikana na hatia ya makosa ya ugaidi. Program ya tisa ya kundi la wahitimu lilimaliza masomo wiki iliyopita. Vyombo vya habari vili alikwa kushuhudia sherehe zao za kuhitimu katika gereza la Sale karibu na mji mkuu Rabat. Kuhitimu kutoka kwenye mpango huo hakufanyi wafungwa wastahiki moja kwa moja kuachiliwa mapema lakini kunaongeza fursa zao za kupata msamaha au kupunguziwa adhabu.
Magenge yenye silaha ambayo yamewateka nyara maelfu ya abiria katika shambulizi la kwenye treni huko kaskazini mwa Nigeria yanatumia raia kama ngao ya kibinadamu na hivyo kufanya iwe vigumu kwa jeshi kutekeleza kazi ya uokoaji Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema Jumatatu. Shirika la reli la serikali ya Nigeria lilisema mwezi uliopita kuwa watu 168 walipotea kufuatia shambulizi la Machi 28.