Rais wa Marekani Donald Trump na mpinzani wake wa Democratic Joe Biden wametumia saa zao za mwisho za mbio za kuelekea Ikulu katika majimbo magumu. Bwana Biden alifanya kampeni Pennsylvania na Ohio, wakati Bwana Trump akiwa Winsconsin, Michigan, North Carolina na Pennsylvania.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, alikamatwa kwa muda na kuachiliwa Jumatatu baada ya polisi kusema wamefanikiwa kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na waupinzani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita. Wanasiasa kadhaa wa upinzani wamekamatwa wakati na baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa.
Wakili mmoja wa Kenya amejisalimisha kwa viongozi wa Uholanzi ili kukabiliana na mashtaka dhidi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC). Wakili huyo anadaiwa kuwahonga mashahidi katika kesi dhidi makamu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama hiyo.