Bw Albanese anatarajiwa kukutana na kiongozi huyo wa China Jumatatu. Ziara hiyo inalengo lakumaliza usitishwaji wa mahusiano yakidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili na, endana na maadhimisho y amiaka 50 ya ziara ya kwanza ya kiongozi wa Australia katika nchi hiyo, iliyo fanywa na Waziri Mkuu wa Labor Gough Whitlam mnamo mwaka wa 1973.
Ripoti mpya kwa afya ya wakimbizi na wanao wasili kwa viza zakibinadam nchini Australia, inaonesha kuwa kuna uwezekano mdogo zaidi kwa jamii kuripoti wanapokuwa na magonjwa kama saratani pamoja na ugonjwa wa afya ya akili. Wakitumia data ya sensa, walipata kuwa wakimbizi na wanao wasili nchini kwa viza zakibanadam walikuwa na uwezekano wa 60% wakuto ripoti matatizo ya pumu na saratani, wanapo linganishwa na umma mpana wa Australia pamoja na kuwa na uwezekano wa 50% yakuto ripoti ugonjwa sugu wa mapafu pamoja na matatizo mengine ya afya ya akili.
Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt amesema serikali inastahili acha idhinisha miradi mipya ya makaa ya mawe pamoja na gesi, kama inatarajia kufikia malengo yake ya kupunguza uzalishaji. Kauli hiyo imejiri baada ya serikali kutangaza inalengo lakutoa 82% ya umeme wa nishati mbadala kufikia 20-30, kutimiza malengo ya makubaliano ya Paris ya uzalishaji sufuri kufikia 2050. Mweka hazina Jim Chalmers amesema miradi ya ziada inaweza tarajiwa katika bajeti ya 2024/25, inayo ongezea kwa mpango wa serikali wenye thamani ya $40 bilioni kuhamia katika nishati mbadala.
Mvua na dhoruba zita ambatana na geuzi linalo karibishwa katika eneo la Western Downs jimboni Queensland, ambako wakaaji wana anza kurejea nyumbani kutazama kilicho baki baada ya moto mubaya wa vichaka. Mtu mmoja alifariki katika moto wa Tara, ambao uli lazimisha mamia ya watu kukimbia pamoja na nyumba 58 kuteketezwa, hizo ni nyumba tisa zaidi zilizo potezwa jimboni Queensland katika mioto ya Black Summer ya 2019. Hekta 26,000 zimechomeka kwa ujumla ila, wazima moto waliweza okoa nyumba 387.
Mkutano wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani umeanza nchini Afrika Kusini siku ya Alhamisi, huku Pretoria na Washington zikirekebisha uhusianowao baada ya mzozo kuhusu shutuma kwamba Afrika Kusini inajihusisha na Russia. Mawaziri kutoka nchi zipatazo 40 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazonufaika na Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika, au AGOA, watafanya mazungumzo ya siku tatu na wajumbe kutoka Marekani huko Johannesburg.
Wadau wa afya nchini Tanzania wanaamini kuwa, bima ya afya inapaswa kutoa fursa sawa kwa kila Mtanzania bila kujali kipato wakati mswaada wa sheria uliopitishwa umeonyesha kushindwa kuyaondoa matabaka yaliyokuwepo kwenye mfuko huo. Siku moja baada ya mswaada wa sheria ya bima ya afya kupitishwa na bunge la Tanzania, wadau hao wa afya wamezitaka mamlaka husika kuangalia upya kipengele cha sheria kinachowawajibisha wale watakaoshindwa kulipia bima hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mfalme Charles na Malkia Camilla Alhamisi aliwatazama wanamaji wa Kenya walichukua mafunzo kutoka kwa wananaji wa Uingereza wakitua kwenye ufuo wa bahari katika siku ya tatu ya ziara yao rasmi katika koloni la zamani la Uingereza. Baada ya siku mbili katika mji mkuu Nairobi, Charles na Camilla alisafiri hadi katika mji wa bandari wa Mombasa, ambao ulikuwa mji mkuu wa awali wa British East Africa.