Afisa mkuu wa afya wa Queensland amesema inashangaz kuwa jimbo hilo, halija rekodi kesi yoyote ndani ya jamii leo. Kulikuwa kesi mbili ndani ya jamii jana na, zote mbili ziliungwa kwa maambukizi yanayo julikana, hali ambayo ilituliza hofu kuhusu maambukizi ndani ya jamii ya kusini mashariki Queensland. Dr Jeanette Young amesema uwezo waku kabili milipuko kutoka kesi ya kwanza, kunaweza elezea mafanikio ya jimbo hilo kudhibiti karibu ya milipuko 50 katika mwezi uliopita.
Vitanda vya ziada katika kitengo cha wagonjwa mahtuti almaarufu ICU, vita funguliwa kote jimboni Victoria wiki ijayo wakati idadi yawatu wanao lazwa hospitalini kwa sababu ya COVID inaongezeka. Kuna zaidi ya wakaaji wa Victoria 476 hospitalini wakiwa na virusi hivyo, watu 98 wakiwa ndani ya ICU na watu 57 wakihitaji msaada wamashine kupumua. Takriban 52% ya wakaaji wa Victoria wenye zaidi ya miaka 16, kwa sasa wame pata chanjo mbili.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi anasema anataka ushirikiano wa kweli na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuchunguza tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono. Amesema tuhuma hizo zinawakabili watumishi wa shirika hilo waliopelekwa kupambana na mlipuko wa Ebola nchini DRC. Msemaji wa serikali Patrick Muyaya amekiambia kituo cha televisheni cha taifa Jumamosi kwamba Rais Tshisekedi ametoa wito huo wa kutaka ushirikiano wa dhati kati ya taasisi na vyombo vya serikali na mashirika ya kimataifa yaliyopewa jukumu la kufuatilia kashfa hiyo.