Mkutano wa bodi hiyo wa leo ni wa kwanza chini ya uongozi gavana mpya Michele Bullock aliye chukua usukani kutoka Philip Lowe. Uamuzi wakuacha viwango vilivyo ni sambamba na matarajio ya soko, licha ya mfumuko wa bei kuongezeka kwa 5.2% katika mwezi wa Agosti. RBA haija tupilia mbali nyongeza katika siku za usoni kwa ajili yakupunguza mfumuko wa bei. Na benki hiyo inataka viwango vyakutokuwa na ajira viongezeke kufikia 4.5% kufikia mwaka ujao kama sehemu ya mpango waku fikisha mfumuko wa bei kati ya 2% na 3%.
Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amewarai wahamiaji wapige kura ya La katika kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza bungeni. Kampeni ya La imesema sauti yawa Australia wa kwanzza ni hatua ya kugawanya naku unda viwango viwili vya uraia kwa misingi ya rangi. Kura za maoni zimeweka kampeni ya La mbele chini ya wiki mbili hadi kura ya maoni itakayo fanywa Oktoba 14. Ila Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema bado kuna uwezekano wakushinda kura hiyo ya maoni.
Moto wa vichaka ambao haudhibiti mwashariki mwa Victoria, umeongezeka mara tatu zaidi wakati mamlaka wana waonya watu waondoke. Moto huo unao sambaa kwa kasi Briagolong ambayo iko katika kanda ya Gippsland imefunika hekta 5,000 jumatatu ila, upepo mkali ume sambaza miali na moto huo kwa sasa una sambaa katika hekta elfu 17.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeridhia chanjo ya pili ya ugonjwa wa malaria kwa watoto, ambayo inaweza kuokoa maisha ya maelfu endapo kutakuwa na uwezekano wa kuziba pengo kubwa la usambazaji na mahitaji. Takriban watoto nusu milioni katika kanda ya Afrika hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huo unaosababishwa na vimelea vinavyoenezwa na mbu.
Wanajeshi 29 wa Niger wameuliwa kufuatia shambulio la kigaidi magharibi mwa nchi, ikiwa ni idadi kubwa ya watu kuuliwa tangu wanajeshi kuchukua madaraka ya taifa hilo mwezi Julai.
Maduka katika eneo la biashara la Kariakoo, jijini Dar es salaam yamefungwa Jumatatu kufuatia moto uliozuka Jumapili asubuhi na kuteketeza maduka kadhaa katika eneo hilo maarufu la kibiashara. Wafanya biashara wa eneo hilo muhimu kiuchumi kwa Tanzania na Afrika Mashariki, wana wasiwasi na mali zao na wameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina kutafuta chanzo cha moto huo.