Ndege za Qatar Airways hufanya safari 28 kila wiki katika viwanja vikubwa vinne vya ndege nchini Australia, pamoja na safari za ziada saba mjini Melbourne. Serikali ya Labor ili kataa ombi la Qatar kupanua makubaliano na Australia, yakuruhusu safari za ziada 21 kila wiki katika viwanja vikubwa vya ndege, akisema itatoa ushindani na ndege za nchini pamoja nakuathiri ajira nchini.
Mwenyekiti mwenza wa mazungumzo ya Uluru Megan Davis, ametoa shukran zake kwa John Farnham kwa kuruhusu kampeni ya Ndio, itumie wimbo wake maarufu 'You're the Voice' kwa video ya kampeni yake. Hiyo ni mara ya kwanza msanii huyo ameruhusu wimbo huo utumiwe kwa sababu ya matangazo. Bw Farnham amesema anatumai matumizi ya wimbo huo, yataongeza uungwaji mkono kwa Sauti yawa Australia wa kwanza bungeni na, italeta mageuzi chanya kwa maisha yawa Australia wa kwanza.
Msemaji wa utawala wa kijeshi wa Gabon alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba wameamua mara moja kufungua tena mipaka ya nchi kavu, baharini na anga kuanzia Jumamosi hii. Jeshi la Gabon lilisema Jumamosi kwamba litafungua tena mipaka ya nchi hiyo iliyofungwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais wa zamani Ali Bongo.
Maelfu ya raia waliandamana katika mji mkuu wa Niger, Niamey Jumamosi wakiitaka Ufaransa iviondoe vikosi vyake nchini humo kama ilivyoamriwa na utawala wa kijeshi ulioingia madarakani baada ya mapinduzi Julai 26.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu likiwemo Human Rights Watch yametoa mwito wa uchunguzi wa haraka na kuchukuliwa hatua kwa viongozi wa jeshi waliohusika na mauwaji ya waandamanaji mjini Goma. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limelaani vikali mauwaji ya makumi ya waandamanaji mjini Goma. Thomas Fessy mtafiti mkuu wa Kongo kwenye shirika hilo amesema vikosi vya usalama nchini Kongo vilifyatua risasi kwenye umati wa watu kwa njia ya ukatili na isiyo halali.