Serikali ya shirikisho imejipata chini ya shinikizo kuchukua hatua za ziada kufunga pengo la jinsia kwa malipo, wakati utafiti mpya wa taasisi ya Australia Institute ume onesha mpango wa awamu ya tatu ya makato ya kodi, itatoa faida idadi ya wanaume mara mbili zaidi kuliko wanawake.
Wasafiri wa reli wa New South Wales wanajiandaa kukabiliana na usumbufu wa usafiri kesho, wakati mazungumzo kati ya chama kinacho wakilisha wafanyakazi wa reli, Tram na Basi na serikali ya jimbo hilo yakitarajiwa kuendelea. Hali hiyo inajiri baada ya kuchelewa kwa safari za baadhi ya reli kwa muda wa dakika 20-30 hii leo Agosti 30. Hatua ya viwanda ya kesho inajumuisha marufuku kwa uendesheaji wamagari ya reli yakigeni.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye anapinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa mwezi huu kwenye Mahakama ya Juu, amesema ataheshimu maamuzi ya mahakama – lakini bado anaamini alishinda.