Waziri wa Ulinzi Richard Marles amesema wazalishaji wa makombora ya masafa marefu nchini ni kipaumbele cha Australia. Tathmini ya mapitio ya mkakati wa ulinzi ilitolewa Jumatatu iliyo pita 24 Aprili, ambako ilipata jeshi la ulinzi la Australia halifai kwa kusudi na ilitaka kukuza uwezo wa usahihi wa mashambulizi kwa masafa marefu.
Wazazi wenye hofu ya wanafunzi wa wakenya walioko katika chuo kikuu nchini Sudan wamekuwa wakifika kwenye ofisi ya kaunti ya Wajir nchini Kenya wakati wakisubiri kwa habari kuhusu watoto wao waliokwama katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Jumla ya watahiniwa 106,955 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaofanyika kuanzia Mei 2 hadi 22 mwaka huu. Mtihani huo utaenda sambamba na mtihani wa ualimu utakaofanyika kati ya Mei 2 hadi 16 mwaka huu ambapo jumla ya watahiniwa 8,906 wamesajiliwa.