Waziri wa huduma za jamii Amanda Rishworth, ametangaza tayari kuwa mafao hayo yakutokuwa na ajira yata ongezwa kwa dola 40 kila wiki mbili kuanzia Septemba.
Uchunguzi umeanza kwa kilicho sababisha ajali ya helikopta ya jeshi, katika visiwa vya Whitsunday jimboni Queensland. Timu ya wachunguzi wa ajali hiyo, ime wasili jimboni Qld kuanza uchunguzi wakati vikosi vyakutafuta nakuokoa vina endelea kupekua eneo hilo kwa mabaki ya helikopta hiyo pamoja na walio kuwa ndani yake.
Wiki ya watu walio potea ime anza kwa juhudi zaku toa uelewa wa watu ambao wame potea kwa muda mrefu na, kumulika kiwewe ambacho wapendwa wao wanao acha nyuma hupitia. Hisia za matumaini, kutoweza kufanya chochote ambacho wapendwa huhisi, huzingatiwa kuwa moja ya aina mbaya ya viwewe na dhidi wanayo pitia wakati kuna huduma chache sana za misaada.
Kumekuwa na maoni mchanganyiko miongoni mwa Wasudan kuhusiana na hatma ya mapigano yanayoendelea kati ya majenerali wawili waliohasimiana. Huku baadhi yao wakiwa na matumaini huenda mapigano yakamalizika na wengine wakiwa wamepoteza matumani ya kurejea kwa amani katika taifa hilo la Afrika.
Mahasimu wakuu wakisiasa nchini Kenya hatimae wakubali kufanya mazungumzo, mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio One Kenya ilitoa taarifa kwa umma kuhusu maamuzi waliyo fikia.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Ijumaa amewasili kwenye mji mkuu wa jimbo la Sichuan, wa Chengdu, kusini-magharibi mwa China, ili kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa michezo ya 31, ya shirikisho la michezo ya vyuo vikuu vya kimataifa, FISU, pamoja na kutembelea China.
Morrocco timu ya pili kutoka Afrika kushinda mechi katika kombe la dunia la FIFA, wenyeji NewZealand watupwa nje na hatma ya Australia i mikononi mwake kesho usiku.