Kiongozi wa zamani wa upinzani katika jimbo la NSW Michael Daley, anataka rejea katika wadhifa wa uongozi baada yakutangaza nia yake, yakuwania uongozi wa chama hicho kwa mara ya pili.Bw Daley alirithi wadhifa huo kutoka kwa Luke Foley karibu ya mwisho wa mwaka wa 2018, kabla yakuongoza chama hicho kushindwa katika uchaguzi wa jimbo hilo wa mwaka wa 2019.
Mweka hazina wa Victoria Tim Pallas, amesema maombi kadhaa ya msaada yame puuzwa na mshirika wake wa shirikisho Josh Frydenberg. Jimbo la Victoria limetangaza mfuko wa msaada wenye thamani ya milioni $250, kusaidia biashara ndogo nazakati takriban elfu tisini, wafanyabiashara binafsi ambao wame athiriwa kwa makatazo yakutoka nje nao pia wame jumuishwa katika mfuko huo wa msaada.
Zaidi ya watu 20 jimboni Tasmania, wame kimbizwa hospitalini baada yakupumua gesi inayo aminiwa kuwa ni carbon monoxide. Tukio hili lilifanyika katika kiwanda cha Tassal salmon karibu ya mji wa Dover, nakuwaacha wengi wakiwa na matatizo yakupumua pamoja nakutapika.