Wafanyakazi wanao wahudumia wagonjwa katika wakati wa dharura jimboni NSW, wauguzi pamoja na wafanyakazi wengine wa huduma ya afya, wana ongeza hatua zao zakuomba nyongeza kwa mshahara wao, baada ya serikali ya Labor kufeli kutimiza ahadi yakuongeza mishahara hiyo miezi mbili baada yakuingia madarakani.
Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema kuwa wa Australia wanao pinga sauti yawa Australia wakwanza bungeni si wabaguzi wa rangi. Kauli hiyo inafuata shutma za kiongozi wa upinzani Peter Dutton dhidi ya waziri mkuu, kuhusu matamshi ya matusi kuhusu mjadala wa the Voice.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu ameishutumu sheria mpya ya Uganda inayopinga mapenzi ya jinsia moja na kusema kuwa inakiuka haki za binadamu, na inahatarisha maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo iliyoko mashariki mwa bara la Afrika.
Kenya itatia saini mkataba wa biashara na Urusi unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, ofisi ya Rais William Ruto ilisema siku ya Jumatatu, baada ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov jijini Nairobi.