Taarifa ya Habari 30 Novemba 2023

City - Swahili.jpg

Maafisa wa Australia wana endelea kuwasaidia watu 67 wanao taka ondoka Gaza ila, wanasema hali huko ni mbaya katika siku ya mwisho ya kusitishwa kwa muda kwa vita.


Maafisa wamefanikiwa kupata njia salama yawa Australia 131 kupitia kutoka, eneo hilo ambalo lime kumbwa kwa makombora tangu mwanzo wa vita. Walio ondoka katika eneo hilo wali lakiwa nama afisi wa Australia katika mpaka wa Misri na, waliwasafirisha hadi katika mji mkuu wa Cairo ambako walipewa vifaa muhimu kama mavazi ya watoto, maziwa yawatoto, makaazi pamoja na msaada wakufika nyumbani.

Naibu Waziri wa maswala yakigeni Tim Watts amesema hali ina endelea kuwa ngumu zaidi kwa wa Australia wengi kuondoka Gaza ila, maafisa wa ubalozi wanafanya wawezavyo kuwasaidia. Wakati huo huo Hamas imewaachia huru mateka wengine 16 katika siku ya mwisho ya makubaliano yakusitisha vita kati ya Israel na Gaza. Kundi hilo lina aminika kuwajumuisha wa Israeli, watu wenye uraia pacha pamoja na raia wa Thailand.

Mazungumzo bado yana endelea kwa ajili yakuongeza muda wakusitisha vita ila, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa Israel ina nia yaku anza vita dhidi ya Hamas muda wakusitisha vita utakapo isha. Shirika la OECD limetoa makadirio yake kwa uchumi wa Australia na, wanatabiri kuwa taifa hili lina karibia kuingia katika mwaka wakuyumba. Shirika hilo lime sema kuna uwezekano ukuaji huo huenda usihisike, kama mfumuko wa bei unaendelea au uchumi wa China una yumba.

Kila jimbo na wilaya nchini Australia ime wekwa katika tahadhari ya juu, baada yakutolewa kwa mtazamo wa mwaka huu wa msimu wa moto wa vichaka.

Baraza la taifa la moto wa vichaka na huduma za dharura, limesema mvua nyingi katika miaka michache iliyopita, imesababisha ukuaji wa majani mengi pamoja na mazingira magumu kumaliza kupunguzwa kwa hatari. Mtazamo huo umesema mazingira hayo, yata endelea kukauka katika sehemu nyingi kote nchini Australia, kujumuisha baadhi ya maeneo yaliyo athiriwa katika msimu wa Black Summer wa 2019-20.

Spika wa bunge la Kenya amepiga marufuku kile alichokieleza kuwa mavazi yasiyofaa yanayovaliwa na wabunge, hata kupiga marufuku vazi la kitamaduni la kiafrika na suti zinazopendwa na Rais William Ruto. Moses Wentan’ugula aliwambia wabunge Jumanne kuwa lazima waheshimu sheria za mavazi za bunge, akikemea “mitindo inayoibuka ambayo sasa inatishia kanuni za mavazi za bunge.” Amesema kile kinachoitwa suti aliyokuwa akipenda kuvaa hayati rais wa Zambia Kenneth Kaunda, limepigwa marufuku pia, pamoja na mavazi ya kitamaduni yasiyofaa. Ruto huvaa mara nyingi suti za kawaida, lakini vazi la Kaunda sasa ndilo vazi lake analolipenda, na alilivaa wakati wa ziara ya Mfalme Charles wa tatu mapema mwezi huu.

Wabunge wa upinzani nchini Uganda wamerudi bungeni baada ya kususia vikao kwa zaidi ya mwezi mmoja. Hii ni baada ya spika wa bunge Anita Among kuwarai huku akimshinikiza waziri wa masuala ya ndani na yule wa usalama kuwasilisha taarifa kuhusu watu wanaodaiwa na upinzani kutoweka baada ya kukamatwa na vyombo vya dola. Spika aliorodhesha suala la wabunge wa upinzani kwa mara ya kwanza kwenye ratiba ya shughuli za bunge na wabunge wa upinzani walipoiona wakakubali kurejea bungeni. Lakini hii ilikuwa baada ya kutokea vurugu chache wakati baadhi ya wabunge wa chama tawala NRM na wengine wa upinzani walipotupiana maneno na kusababisha polisi wa bungeni kuingilia kati kuidhibiti hali.

Katika michezo, wachezaji wamekataa toleo kutoka shirika la Netball Australia kwa ajili yakumaliza sintofahamu ya muda mrefu ya malipo, wakisema toleo hilo linge walazimisha wachezaji kurejea kazini wakati, sehemu mhimu ya mfumo wa ushirikiano bado unajadiliwa.   Netball Australia ilitumai kufikia mwisho wa mvutano huo kwa kutoa nyongeza ya mshahara ya 11% ambayo ingelipwa kurudi nyuma katika tarehe 1 Oktoba na, kukubali kwa mara ya kwanza kuchangia kwa mapato.   Hata hivyo, shirika linalo wakilisha wachezaji wa mchezo wa pete nchini, limesema wachezaji hawata rejea kazini hadi masharti ya ushirikiano yakamilishwe.   Wanataka 15% ya mapato zaidi ya kinacho tabiriwa kutoka kwa wafadhili wapya.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 30 Novemba 2023 | SBS Swahili