Chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Victoria, ujenzi wa mapema umeanza katika barabara yaku elekea uwanja wa ndege wa Melbourne. Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews, ametangaza uwekezaji wa dola milioni 143 kukarabati kituo cha Sunshine ili kiwe sehemu mhimu yakubadilisha treni katika barabara ya reli ya kanda ya Victoria. Amesema uwekezaji huo ulikuwa tangazo la serikali, si ahadi ya uchaguzi.
Wanafunzi wa elimu ya juu, na wanafunzi wanao somea kazini kutoka kanda la New South Wales, hivi karibuni wataweza pata $250 za usafiri bure kupitia kadi mpya inayo fadhiliwa na serikali ya jimbo hilo. serikali ya jimbo hilo imezindua kadi itakayo kuwa na hela, kusaidia kupunguza gharama ya usafiri kwa vikundi hivyo, kadi hiyo itasaidia kulipia usafiri wa umma, malipo ya taxi au petroli. Kadi hiyo itapatikana kuanzia mwaka ujao, na itatumiwa kwa miaka mbili ya majaribio.
Mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 yaliongezeka karibu na ujirani wa Rutshuru na Kiwanja siku ya Jumamosi, huku milio ya risasi ikizuka wakati wa asubuhi.
Waasi wameteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo baada ya mapigano makali siku ya Jumamosi, na kuongeza maradufu eneo wanalolidhibiti sasa, kiongozi wa mashirika ya kiraia na wakaazi wamesema.