Wanasiasa watarejea bungeni kesho, uponaji wa Australia kutoka janga la COVID-19 ikiwa kipaumbele kwenye ajenda. Wanasiasa hao wanarejea bungeni wakati serikali imethibitisha mipango yake yaku sitisha, marupurupu ya JobKeeper kuanzia Machi, wakati idadi yawa Australia milioni 2.1 hawapokei tena malipo hayo.
Wabunge kadhaa wa Marekani hivi karibuni wamepokea vitisho kwa maisha yao, wakati Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi akitaka usalama uimarishwe katika Bunge la Marekani na kudai kuwa kuna hatari inayokuja siyo tu kutoka uraiani lakini kutoka kwa “adui wa ndani” ya Bunge lenyewe.
Wasiwasi unaongezeka nchini Tanzania kuhusu kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona licha ya matamshi ya serikali kukanusha kwamba ugonjwa huo haupo nchini humo. Kwa karibu mwaka mzima Tanzania imedai hakuna corona nchini humo, na kuwa nchi pekee Afrika Mashariki ambayo haina masharti rasmi ya kujikinga na ugonjwa huo.