Serikali ya Magharibi Australia inawapa baadhi ya wafanyakazi 6% ya nyongeza ya malipo, kama kinga dhidi ya mfumuko wa bei. Idadi ya wafanyakazi 150,000 katika sekta ya umma, wanao jumuisha walimu, wauguzi maafisa wa jeshi la polisi, wanao fanya usafi pamoja na watumishi wa umma, kwa sasa wanapewa nyongeza ya 3% kwa mshahara wao kwa muda wa miaka miwili ijayo.
Marekani imeiomba serikali ya DRC kuwalinda walinda amani wa Umoja wa Mataifa na majengo yao kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo. Maandamano ya kuipinga Tume ya UN nchini humo, inayojulikana kama MONUSCO, yamezuka tangu Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 19 ikiwemo walinda amani wa UN watatu.
Kura mpya ya maoni ya shirika la utafiti la Tifa lenye makao yake mjini Nairobi inaonyesha kuwa kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya kiko sawa ki takwimu. Raila Odinga kiongozi wa upinzani anayewania nafasi hiyo kwa mara ya tano, anaongoza kwa asilimia 46.7 na mpinzani wake William Ruto naibu rais wa sasa ana asilimia 44.4 ya kura. Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ili kushinda katika duru ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu, mgombea ana hitaji zaidi ya nusu ya kura zote angalau asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo takriban nusu miongoni mwa yote 47.