Anthony Albanese amehotubia mkutano wa chama cha Labor kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu, na amewathibitishia wanachama kuwa chama cha Labor kita ongoza serikali ya wengi baada chama tawala kushinda viti 77 bungeni.
Sehemu za kazi nchini Australia zina hamasishwa ziongeze juhudi, kuwasaidia wahanga wa unyanyasaji wa nyumbani. Na wakaaji wa Victoria watastahiki kupata chanjo za mafua bure katika mwezi ujao wa Juni. Jimbo la Victoria limejiunga na New South Wales, Kusini Australia, Magharibi Australia na Queensland, kutoa chanjo za mafua bure kwa wakaaji katika mwezi mzima wa Juni.
Mamia ya watu waliandamana dhidi ya Rwanda siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa kuhusu shutuma kuwa Kigali inaliunga mkono kundi la waasi la M23 huku mivutano kati ya majirani hao wawili ikiongezeka. Waandamanaji hao pia walitoa wito wa kufukuzwa kwa balozi wa Rwanda nchini DRC na kubeba mabango yenye kuonyesha uzalendo wao. Congo ni nchi yetu, hakuna hata sentimita moja itakwenda Rwanda, moja ya bango lilisomeka hivyo.