Idadi ya wagonjwa wapya wanao hudumiwa katika taasisi yautaalam mkubwa duniani ya Melanoma nchini Australia, imepungua kwa muda wa miaka 12, nakusababisha hofu miongoni mwa wataalam kuwa vizuizi vya COVID vime wazuia wagonjwa kufanya vipimo vya ngozi. Kuna wasiwasi kupungua kwa 20% ya wagonjwa wapya katika miaka mbili iliyopita, kuna weza shuhudia ongezeko kwa maisha yanayo potezwa kwa sababu ya ugonjwa huo katika miaka ijayo.
Taarifa ya Habari 31 Oktoba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili
Kiongozi wa chama cha Nationals ambaye pia ndiye kaimu waziru mkuu Barnaby Joyce, ameweka wazi baadhi ya taarifa ambayo chama chake kili afiki na chama cha Liberal, kuafiki kupunguza uzalishaji wa hefa chafu kwa kiwango cha sufuri kufikia mwaka wa 2050, ambayo ilijumuisha uwekezaji kwa kanda kusaidia katika mageuzi hayo.
Share