Wafanyakazi wa muda ambao hawataki hamia katika mikataba yakudumu, hawata lazimishwa kuwa na mikataba hiyo baada ya serikali kukubali kurekebisha muswada wa mageuzi ya kazini. Hali hii imejiri wakati baadhi ya sekta, zinazo jumuisha migahawa na maduka ya rejareja, ilizua wasiwasi kuwa wafanyakazi wa muda wata lazimishwa katika mikataba ya kufanya kazi kwa masaa mengi, hali ambayo inge ondoa mafao yao pamoja na faida zingine.
Ziara ya mfalme Charles wa Uingereza imezua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya, ambao baadhi yao wanaiona ziara hiyo kuwa fursa nzuri ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili. Huku baadhi ya Wakenya wakijiandaa kufanya maandamano kudai fidia kutokana na dhuluma zilizofanywa na wanajeshi wa Uingereza katika kambi ya jeshi ya Nanyuki. Lakini baadhi ya Wakenya wamesema watafanya maandamano siku ya Jumanne kupinga ukatili waliofanywa na baadhi ya wanajeshi katika kambi ya Nanyuki pamoja na kuulalamikia utawala wa kikoloni. Mfalme Charles anaanza ziara yake ya kwanza kama mfalme katika taifa la Jumuiya ya Madola, ambapo maoni yoyote atakayotoa juu ya historia ya ukoloni wa Uingereza yatafuatiliwa kwa karibu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametupilia mbali miito ya usitishwaji mapigano dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza. Netanyahu amesema wito wa usitishwaji mapigano ni sawa na kuitaka Israel kujisalimisha kwa kundi la Hamas na kuafiki ugaidi na ukatili. Amesema hilo haliwezekani na kunukuu Biblia kwamba kuna wakati wa amani na wakati wa vita, na kwamba sasa ni wakati wa vita ili kuandaa mustakabali wa pamoja.