Ombi hilo limejiri wakati mamlaka kuu za afya za serikali, zinachunguza sababu na viungo kati ya chanjo ya AstraZeneca, iliyo chukuliwa na mwanaume mmoja kutoka Melbourne mwenye miaka ya arobaini, pamoja na hali yake isiyo yakawaida yakuganda kwa damu.
Chama cha upinzani cha shirikisho kime omba pawe uwazi zaidi kwa data, inayotolewa kuhusu utoaji wa chanjo nchini Australia. Kufikia wikendi hii, idadi yawa Australia ambao wamepokea angalau dozi moja ya chanjo ya coronavirus ni 841,885.
Wa Australia walio hudhuria ibada za pasaka mapema leo Jumapili, wamesema kuna hali maalum ya shukrani mwaka huu. Mwaka moja uliopita, kanisa nyingi na sehemu za ibada zilifungwa kwa sababu ya hali ya dharura ya afya ya umma.
Kenya imetangaza jana kuzuiia kampuni binafsi kuingiza chanjo za virusi vya corona nchini humo ikisema ina wasiwasi kuwa chanjo bandia zinaweza kupelekwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.Taarifa iliyotolewa na Kamati ya taifa ya kushughulikia janga la virusi vya corona nchini Kenya imesema, amri hiyo itaendelea hadi pale mchakato wa kununua chanjo kupitia kampuni binafsi utakapokuwa wa uwazi na uwajibikaji.
Kundi la wanamgambo la al-Shabaab limefanya mashambulizi dhidi ya Jeshi la Somalia katika mkoa wa Lower Shabelle, maafisa wa mkoa wamesema. Mashambulizi hayo yamefanyika Jumamosi asubuhi, majira ya saa kumi alfajiri kwa saa za Somalia, yakilenga kambi za jeshi katika miji ya Barire na Awdhegle kusini mwa Somalia.