Serikali ya Victoria imesema inalengo laku unda nguvu kazi jumuishi kwa wanawake, na jamii yawa Australia wa kwanza kwa sababu mradi wa mzunguko wa reli wa vitongoji vya Mashariki, unatarajiwa kuunda zaidi ya ajira 800. Mradi wa Rail Loop East, utaruhusu iadi ya safari za ziada milioni 11.8 kila siku nakusimamia ongezeko la 80% katika safari za gari binafsi.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amewasili New York ili kujisalimisha kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai yanayotishia kukitikisa pakubwa kinyang'anyiro cha urais wa Marekani katika uchaguzi wa mwaka 2024.
Takriban watu sita wamefariki dunia na wengine darzeni hawajulikani walipo, baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kupinduka kutokana na upepo mkali kwenye Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mamlaka ya eneo hilo ilisema Jumatatu.
Viongozi wa michezo ya AFL na NRL nchini, wafika mbele ya kikao cha seneti kujibu maswali kuhusu kamari katika michezo yao, na walimu kadhaa wa soka katika ligi kuu ya Uingereza wafutwa kazi baada ya matokeo mabaya.