Taarifa ya Habari 4 Disemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya Albanese yatarajiwa kuwasilisha mipango kwa serikali zamajimbo na mikoa kwa lengo laku punguza bili za nishati kwa kuweka kikomo kwa bei ya makaa yamawe yanayo uzwa nchini.


Waziri wa NDIS Bill Shorten amesema anafanya kazi na serikali zamajimbo na mikoa, kuwaondoa watu wengi zaidi ambao wana ulemavu nje ya hospitali nakuwarejesha nyumbani kusherehekea krismasi.

Usalama ufukweni ume ongezwa katika mtaala kwa wanafunzi wakimataifa, baada ya Australia kurekodi mwaka wake mubaya zaidi wa vifo vyakuzama katika fukwe tangu rekodi zilipo anza hifadhiwa. Ripoti ya 2022 ya usalama wa fukwe zakitaifa ilipata idadi ya watu 141 walizama majini katika miezi 12 hadi juni, na takriban nusu ya wote walio fariki walizaliwa ng'ambo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema hana nia ya kujiuzulu na kwamba ataendelea kupambania mamlaka yake na ataipinga ripoti ya bunge mahakamani. Kwa mujibu wa msemaji wake rais huyo anayekabiliwa na kashfa na kitisho cha kuondolewa madarakani hana nia ya kujiuzulu na kwamba ataendelea kupambana kisiasa na kwa njia za kisheria.

Wizara ya Ulinzi ya Somalia inasema jeshi la taifa la nchi hiyo, likisaidiwa na wanamgambo wa koo, wamekamata udhibiti wa vijiji kadhaa vya kimkakati kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam wa al-Shabab. Wizara hiyo imekiri kwamba wana usalama kadhaa walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo ya karibuni ya kijeshi.

Gwiji wa Brazil Pele, asema yuko 'imara na mwenye matumaini mengi', licha yaripoti kutolewa kuwa ameanza kupokea huduma ya mwisho wa maisha na Socceroos waondoka katika kombe la dunia kibabe.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service