Taarifa ya Habari 4 Julai 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri wa Fedha akaribisha uamuzi wa benki ya hifadhi wakuto ongeza kiwango cha riba.


Utafiti mpya umebaina kuwa watu wenye majina ya mwisho yakiingereza, wana uwezekano bora wakupata nafasi za uongozi kuliko wenye majina yakiasili.

Kumekuwa vurugu za hapa na pake nchini Ufaransa usiku wa kuamkia leo lakini pia dalili kuwa maandamano yenye ghasia ambayo yameikumba nchi hiyo kwa siku kadhaa yanapungua. Wizara ya mambo ya ndani imesema ni watu 49 pekee waliokamatwa kufikia usiku wa manane, ikiwa ni idadi ndogo zaidi ikilinganishwa na siku zilizopita.

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza Jumatatu kwamba hatogombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwaka ujao wa 2024, na kumaliza miaka kadhaa ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake wa kisiasa ambao umepelekea kuchochea maandamano ya upinzani mwezi uliopita nchini mwake.

Mahakama Kuu nchini Tanzania kanda ya Mbeya Julai 20 mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi kusikiliza kesi ya kikatiba ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari, iliyofunguliwa na baadhi ya wananchi mkoani Mbeya. Wananchi hao wanadai wana wawakilisha wenzao wanaopinga baadhi ya vipengele vya mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es salaam, nchini Tanzania, kati ya serikali na kampuni ya uwekezaji kutoka Dubai ya DP World.



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 4 Julai 2023 | SBS Swahili