Taarifa ya Habari 4 Oktoba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mweka hazina wa taifa asisitiza kuwa serikali bado haija badili msimamo wayo kwa makato ya kodi ya awamu ya tatu, licha ya ukosoaji kwa mpango huo kutoka upinzani na wadau wengine.


Hatimae Optus imelipa shirika la Services Australia data iliyo omba karibu wiki mbili baada ya ukiukaji mkubwa wa data ambao umewahi tokea, ulio wekwa wazi na serikali kuomba taarifa hiyo. Shirika hilo la serikali sasa, linachunguza data hiyo kuona kile ambacho kinaweza bainika kupitia taarifa hiyo. Optus imerekebisha makadirio yake kwa wateja walio athiriwa, wakisema ni wateja elfu hamsini ambao taarifa zao za Medicare ziliathiriwa, na pasi 150,000 pia zilizo athiriwa.

Wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali siku ya Jumatatu walilenga makao makuu ya serikali ya Somalia katika eneo la Hiran, na kuuwa watu 20 na kujeruhi wengine 36. Hayo yalitokea katika mji ulio katikati ya harakati za hivi karibuni dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali, maafisa na mashahidi walisema. Serikali ya Somalia mapema Jumatatu ilitangaza kwamba ikiwa na washirika wa kimataifa wamemuua kiongozi mkuu wa al-Shabab, Abdullahi Nadir, mwishoni mwa juma.


Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa Ebola nchini Uganda imeongezeka hadi kufikia tisa, wizara ya afya ilisema Ijumaa, wiki mbili baada ya mamlaka kutangaza janga hilo katikati mwa nchi. Idadi mpya ya wagonjwa iliongezeka kutoka saba, takwimu iliyotolewa Ijumaa ilionyesha. Mwezi uliopita wizara ya afya ilitangaza kifo cha kwanza katika taifa hilo lisilo na bandari kutokana na virusi hivyo, ambavyo viliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019, na kutangazwa kuzuka katika wilaya ya kati ya Mubende.





Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 4 Oktoba 2022 | SBS Swahili