Bw Dutton amesema hatakama haungi mkono kura hiyo ya maoni, atatoa fursa kwa wa Aboriginal sauti zao zisikizwe kupitia kura ya pili ya maoni.
Seneta wa chama cha Nationals Bridget McKenzie ameomba uchunguzi ufanywe kwa uamuzi wa serikali ya shirikisho, kukataa ombi la safari za ziada za kampuni ya ndege ya Qatar Airways. Seneta McKenzie amewasilisha tayari ombi rasmi la utoaji wa haki za umma zinazo husiana na uamuzi wa Waziri wa usafiri Catherine King. Hatua yakuzuia safari za ziada 21 imekosolewa baada ya taarifa kuvuja kuwa kampuni ya ndege ya Qantas, ilikuwa ime irai serikali isitoe idhini hiyo kabla yakurekodi faida ya $2.5 bilioni katika mwaka wa fedha wa 2022/23. Seneta huyo ameongezea kuwa, safari hizo za ziada za ndege ya Qatar, zilikuwa na uwezekano wakupunguza nauli za ndege pamoja nakupiga jeki sekta ya utalii ya Australia.
Wanaharakati wa ustawi wa watoto, wameiomba serikali ya shirikisho ianzishe kongamano lakujadili njia bora yakuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji na unyonyaji. Shirika lakitaifa lakuzuia unyanyasaji nakupuuza watoto, limetumia uzinduzi rasmi wa wiki ya ulinzi wa watoto ambayo imeanza hii leo, kutoa wito kwa mazungumzo mezani kupitia barua rasmi kwa Waziri mkuu Anthony Albanese. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Leesa Waters, amesema umakini zaidi unahitajika wakati 3% kati ya 5% au 60% yawa Australia wamepitia uzoefu wa aina moja ya unyanyasaji iwapo ni kimwili, kihisia, kupuuzwa au hata kingono. Wito wa shirika hilo umefika wakati mmoja na wito kutoka Polisi wa shirikisho ambao wana omba umma msaada, kutatua kesi kadhaa za visa vya unyanyasaji wa watoto ambavyo havija tatuliwa.
Maelfu ya watu nchini Niger, Jumapili waliandamana kwa siku ya tatu mfululizo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Niamey, wakimtaka mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa kuondoa wanajeshi wake, kama inavyotaka serikali ya kijeshi, iliyonyakua mamlaka mwezi Julai. "Ufaransa ishindwe! Ufaransa, iondoke," waandamanaji hao waliimba, wakirudia kauli mbiu zilizosikika katika mikutano mbalimbali, tangu mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 26 mwezi Julai. Utawala wa kijeshi wa Niger, Ijumaa uliishutumu Ufaransa, kwa kile ulichokiita"uingiliaji wa wazi" wa masuala ya ndani ya nchi hiyo, kwa kumuunga mkono rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum.
Watu wawili waliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati gari lao lilipovamiwa na watu wenye silaha magharibi mwa Burundi karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakazi walisema Jumapili. Watu wawili waliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati gari lao lilipovamiwa na watu wenye silaha magharibi mwa Burundi karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakazi walisema Jumapili. Shambulio hilo lilitokea katika barabara ya kutokamkoa wa Bubanza kuelekea mji mkuu wa kibiashara wa Burundi, Bujumbura, Wakazi walisema.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kwamba anatafakari kuhusu hatua kali za kuchukua zikiwa ni pamoja na kuwarejesha makwao wahamiaji baada ya maandamano yaliyogeuka ghasia mjini Tel Aviv. Makundi hasimu ya raia wa Eritrea yalizua ghasia kutokana na misimamo tofauti ya kisiasa ya nyumbani kwao, ambapo baadhi walijeruhiwa pamoja na uharibifu kwa mali. Maandamano yaligeuka ghasia katika mitaa ya Tel Aviv baada ya mamia ya raia wa Eritrea wanaoiunga mkono serikali yao, pamoja na wale wanaoipinga. Maandamano ya jumamosi yalifanyika wakati wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kiongozi wa sasa wa Eritrea kuingia madarakani, wakati wanaoipinga serikali wakiwa wamevaa mashati ya bluu mfano wa bendera ya taifa hilo ya 1952, ikiwa ishara ya kupinga utawala wa kidikteta.
Katika michezo, Arsenal wamepata ushindi wa dakika ya mwisho dhidi ya Manchester United mjini London, hatua ambayo ime waweka katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Uingereza. Wageni hao kutoka Manchester walifunga goli la kwanza kupitia Marcus Rashford katika dakika ya 27 ila, dakika moja baadae Martin Odegaard alifunga goli lakusawazisha katika mechi hiyo. Mechi hiyo ilikuwa inaelekea kuisha kwa sare yakufungana, ila kiungo mpya wa Arsenal Declan Rice alifunga goli la pili katika dakika ya sita ya ziada. Naye Gabriel Jesus aligonga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Manchester United katika dakika ya 11 ya nyongeza nakuwa wenyeji ushindi wa magoli matatu kwa moja.