Kampuni moja inayo toa huduma ya wazee mjini Melbourne ambako watu 45 walifariki kwa wasababu ya UVIKO-19, imefunguliwa mashtaka na huduma inayo chunguza usalama wa kazini, wakati baadhi ya wanachama wa familia husika wana amini ma meneja wa makazi hayo wanastahili fungwa jela. Jana Jumatatu WorkSafe Victoria, ilitangaza kuwa imefungua mashtaka dhidi ya kampuni ya St Basil's Homes for the Aged jimboni Victoria, kwa makosa tisa ya sheria ya afya na usalama kazini.
Jeshi la Uganda UPDF limeongeza mashambulizi dhidi ya waasi wa kundi la kiislamu la allied democratic forces - ADF, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Roketi na mizinga mizito inaendelea kufyatuliwa, ikilenga kambi za ADF baada ya taarifa za ujasusi kwamba waasi wa ADF wamekuwa wamejikusanya na kuunda kambi kadhaa kivu kaskazini. Oparesheni ya jeshi la Uganda nchini DRC kwa jina Shujaa, ilianza Novemba mwaka uliopita, lakini ilisitishwa kwa mda baada ya ruhusa ya serikali ya DRC kumalizika mwezi mwezi May kabla ya DRC kuingia na Uganda makubaliano mapya.
Mauaji ya watu sita yaliyofanywa na mtu aliyejihami kwa bunduki huko Chicago, Marekani Jumatatu, yametilia kiwingu maadhimisho ya siku ya uhuru yanayofanyika kote nchini humo.Tukio hilo limejiri katika wakati ambapo nchi hiyo tayari iko kwenye tafrani ya maamuuzi ya mahakama ya juu kuhusiana na uavyaji mimba na umiliki wa bunduki na pia jaribio la mapinduzi la Januari 6 katika majengo ya bunge.