Chama cha wafanyakazi wa huduma ya afya kimekaribisha ahadi ya uwekezaji kutoka serikali ya NSW, kuajiri wasaidizi wapya wa dharura pamoja nakutoa rasilimali kwa vituo 30 vya gari za dharura. Takriban wasaidizi wapya 2,000 wa huduma ya dharura, wata ajiriwa kufanya kazi katika huduma ya dharura ya New South Wales chini ya mpango huo. Itagharimu bajeti $1.76 bilioni katika miaka minne, pamoja na hela taslim kwa wafanyakazi wa gari za dharura 210, wauguzi 52 pamoja namadaktari wanane.
Viongozi wa jumuia ya maendeleo ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wanakutana mjini Accra Ghana Jumamosi kwa lengo la kuzungumzia na kuamua ikiwa wapunguze au waongeze vikwazo dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Guinea. Rais Nana Akufo Ado akifungua mkutano huo amesema, nia yao ni kutafuta njia za kutathmini na kutafakari juu ya hali katika nchi hizo tatu na kutafuta njia za kuzisaidia kurudi kwenye utawala wa kikatiba chini ya raia.
Baba wa binti wa miaka 10 aliyeuawa huko Uvalde, Texas, katika shambulizi la bunduki na mfanyakazi mmoja wa shule wamechukua hatua za awali ambazo zinaweza kupelekea mashtaka dhidi ya Daniel Defense, mtengenezaji wa bunduki zilizotumika kushambulia na kuwaua watu 21. Daniel Defense ya huko Black Creek, Georgia, haikujibu haraka ombi la kutoa maoni yao.