Jimbo la Victoria limerekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya Uviko-19 katika siku moja, tangu mwanzo wa janga la Uviko-19. Dazeni yawafungwa na walinzi wamagereza ni miongoni mwa zaidi ya kesi 14000 za coronavirus zinazo hudumiwa jimboni Victoria.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na familia yake ni miongoni mwa viongozi wa dunia wanaosemekana kuwa wameficha mabilioni ya dola katika akaunti za siri nje ya nchi. Rekodi ilizopata jumuiya ya kimataifa ya wanahabari wa uchunguzi, zinaonyesha kwamba familia ya Kenyatta ina utajiri wa dola nusu bilioni, uliohusishwa katika angalau taasisi saba na katika nchi mbali mbali. Fedha hizo zinadaiwa kuwekwa nchi ambazo hazitozwi kodi ikiwemo Panama, British Virgin Islands.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameapishwa leo kuongoza muhula wa pili, huku viongozi wachache wa Afrika waliohudhuria hafla hiyo wakimuhimiza kuliweka pamoja taifa hilo linalokabiliwa na vita vya miezi 11 katika jimbo la kaskazini la Tigray.