Kumekuwa vifo vingine vitatu, vyote vikiwa katika maeneo ya Magharibi na kusini magharibi Sydney. Watu hao ni watu wawili ambao walikuwa hawaja chanjwa na walikuwa na magonjwa mbali mbali, na mwingine alikuwa amepokea dozi moja tu ya chanjo. 40% ya wakaaji wote wanao stahiki kwa sasa wamepokea chanjo kamili, wakati 73% yawakaaji jimboni humo wame pokea dozi moja ya chanjo.
Vizuizi jimboni Victoria vinaweza regezwa mapema kuliko ilivyo ratibiwa, wakati 60% ya wakaaji wa Victoria wanapokea dozi yao ya kwanza ya chanjo. Jimbo hilo lilirekodi kesi mpya 183 za coronavirus na 82, ambazo hazija ungwa na milipuko inayo julikana. Mzunguko wa kilomita 5 uta ongezwa, wakati wa ziada wa mazoezi utaruhusiwa na kufunguliwa tena kwa vifaa vya kufanyia mazoezi nje, punde jimbo hilo litakapo fikia 70% ya dozi ya kwanza ya chanjo.
Polisi Tanzania imesema Ijumaa walikuwa wanachunguza madai dhidi ya baadhi ya maafisa wa polisi kuhusika na ubakaji na udhalilishaji wa kingono wa wanawake kadhaa katika vilabu vya usiku. Hatua hii ni kufuatia kusambaa madai hayo ambayo yalisababisha malalamiko na wito wa kuchukuliwa hatua za haraka. Shutuma hizo zimetolewa wakati wa mkutano wa hadhara na kamishna wa polisi wa wilaya ya Handeni, katika mkoa wa Tanga wiki hii.